20 Oktoba 2023 - 19:53
Holocaust ya karne mara hii yatekelezwa Gaza

Wakati dunia ingali katika mshangao wa kushambuliwa kwa mabomu hospitali iliyojaa Wapalestina waliojeruhiwa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel, mashambulizi makali ya anga na makombora ya utawala huo yangali yanaendelea dhidi ya Ukanda mzima wa Ghaza kwa wiki ya pili mfululizo.

Mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Hospitali ya al-Maamadani ya Ghaza na mauaji ya kutisha ya wanawake, watoto na wazee yanahesabiwa kuwa jinai kubwa zaidi ya kivita na mauaji ya kimbari katika karne hii.

Wahanga hao aidha walienda hospitali kuwahudumia majeruhi wao, au walidhani kwamba mahali hapo palikuwa salama kutokana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni kwa mujibu wa kanuni za kimataifa.

Kwa mujibu wa uthibitisho wa Wizara ya Afya ya Palestina, wahanga wote wa mashambulizi ya kinyama ya Wazayuni katika Hospitali ya Al-Maamadani katika Ukanda wa Gaza walikuwa raia wa kawaida.

Katika historia, nchi zinazopigana daima zimekuwa zikizingatia viwango vya chini zaidi vya sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na kulindwa hospitali na vituo vya matibabu dhidi ya mashambulizi, lakini utawala haramu wa Israel hauzingatii sheria zozote za kimatifa, ambapo sasa kufuatia malalamiko makubwa ya jamii ya kimataifa, unafanya juhudi za kufunika jinai hiyo na kujiondolea lawama kuhusiana na shambulio hilo la kinyama dhidi ya watu wasio na hatia.

Inaonekana kwamba Wazayuni wametegemea sana kitabu chao cha Talmud katika kutekeleza jinai za kiholela dhidi ya Wapalestina kwa sababu kwa mujibu wa maandiko ya kitabu hicho, mtu yeyote asiye Myahudi anapasa kuuawa, hata kama atakuwa ni mwema na msafi kiasi gani."